Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt.Mwanakhamis Adam Ameir amesema, katika kusimamia vizuri majukumu ya kila siku ipo haja ya kuendelea kupatiwa mafunzo mbalimbali yanayoweza kuwajengea uwezo Walimu kufikia malengo ya sekta ya Elimu nchini.
Amesema hayo wakati akifunga kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ocean view kilimani Mjini Magharibi Unguja.
Amesema, Mafunzo ya mara kwa mara huengeza ujuzi kwa walimu kuweza kusomesha kwa bidii.
Aidha amesema , Walimu Wakuu wao ndio wasimamizi wakuu ili kuhakikisha Zanzibar itaendelea kupata matokeo mazuri zaidi.
Amesema, ili Taifa liendele kupata matokeo bora zaidi kunahitajika usimamizi mzuri kwa kila mtu kwanzia Mwalimu Mkuu hadi Mwanafunzi.
Akizungumzia suala la mageuzi ya elimu nchini amesema , inasisitizwa kila Skuli lazma iwe na Tathmini ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata fursa ya elimu Amali husika kutokana na matokeo yake.
Mapema Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar Bi. Maimuna Fadhil Abass amesema , kutokana na mafunzo mbalimbali yanayoendelea kutolewa imewasadia sana Walimu na kupelekea kuengaza bidii ili kuhakikisha lengo la kuondosha zero linafikiwa.
Nae Meneja Muandamizi wa Mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar Ndugu . John Massenza amesema , kutokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya 8 Sekta ya Elimu , inaendelea kuimarika kwa kupata ufaulu mzuri hasa kwa masomo ya sayansi.
Amesema , Serikali imehakikisha inaboresha miundombinu na kuwajengea uwezo wa umahiri Walimu ili kuengeza kiwanga cha ufaulu nchini.