Amesema hayo Meneja Rasilimali watu Tawala na Mipango Bi. Khadija Masoud Haji ambae pia kaimu Mkurugenzi wa bodi ya Huduma za Maktaba, akizungumza na Balozi wa Marekeni nchini Tanzania huko ofisini kwake Mjini Unguja.
Amesema, Ili kuweza kusonga mbele katika Sekta ya Elimu basi ipo haja ya kuwa na mashirikiano mazuri na wadau mbali mbali wa Elimu.
Amesema, Bodi ya huduma za Maktaba Zanzibar, bado inahitaji mashirikiano ya kutosha ikiwemo upatikanaji wa Vifaa ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii.
Aidha, Bi khadija ameushukuru Ubalozi wa Marekeni kwa kuwaletea Wakufunzi wenye taalamu katika uendeshaji bora wa huduma za Maktaba.
Kwa Upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Michael A Battle, amesema, lengo la ujio wao ni kuja kuaangalia Mazingira wanayo fanyia kazi Wakufunzi wao, pamoja na kujenga mahusiano mazuri kwa wafanyakazi wa Bodi ya Huduma ya Maktaba ili kuweza kuwasadia katika swala zima la Elimu.
Nae Mkufunzi kutoka Marekani ambae anaisadia bodi hiyo katika uendeshaji wa Maktaba Bi. Tegan Mcroberts amesema, amefurahi kufanya kazi katika Maktaba hiyo na kuahidi kuzidisha mashirikiano ili lengo liweze kufikiwa.