Serikali kupitia wizara ya elimu inafanya kila jitihada ili kuhakikisha inaondosha kabisa alama ya zero kwenye matokeo ya kidato cha nne.
Amesema hayo Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bi Asya Iddi Issa wakati wa mkutano na Walimu Wakuu wa Skuli zenye Wanafunzi wengi wa kidato cha nne katika ukumbi wa Mikutano wa Mazizini Unguja.
Akizitaja skuli ambazo zinaongoza kuwa na wanafunzi wengi amesema ni skuli ya Mwanakwerekwe C 410, Mtopepo 416, Kinuni 400 , na Nyerere 483.
Amesema idara yake ipo sambamba na Walimu hao ili kuendelea na mikakati ya kuhakikisha Skuli hizo nazo zinaondoa kabisa alama ya zero.
Bi Asya amesema kutokana na changamoto ya wingi wa wanafunzi kwenye baadhi ya Skuli za Mkoa wa Mjini Magharibi idara kwa kushirikiana na Walimu hao wataendelea na bidii kuhakikisha wanafunzi wote wanapata ufaulu mzuri na kuondosha kabisa alama ya zero.
Aidha bi Asya amesema wazazi nao wananafasi ya kushikiana na walimu ili kuhakikisha jitihada hizo zinapelea wanafunzi matokeo mazuri.
Pia Mkurugenzi Asya amewataka walimu hao kuhakikisha wanadhibiti utoro kwa kuchukua hatua na kupeleka taarifa kwa Katibu Mkuu ili zichukuliwe hatua kama ilivyoelezwa na baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) na kuhakikisha taarifa hizo ziwe sahihi na ziwe na vielelezo vilivyojitosheleza.
Nao walimu walioshiriki kikao hicho wamesema utoro ni changamoto kubwa kwa wanafunzi hao na kupelekea wao kupata matokeo mabaya.
Wamesema utoro huo huzidi kipindi ambacho wanafunzi kusajiliwa na kuhakikisha watafanya mtihani wa taifa
Kikao hicho cha tatu kimefanyika leo tarehe 13/09/2023 ni muendelezo wa kuweka mikakati ya kuondosha alama ya zero hasa katika skuli zenye idadi kubwa ya wanafunzi.