Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw.Khamis Abdulla Said leo tarehe 18/01/2024 amekutana na kufanya mazungumzo na walimu Wakuu wa Skuli za Maandalizi, Msingi na Sekondari wa Mjini Magharib katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari  Haile  Selassie Iliyoko Wilaya ya Mjini Unguja.

Lengo la Mazungumzo hayo ni kuwataka Walimu hao kuzidisha kasi na nguvu kwa walimu wao ili waweze kuongeza jitihada katika ufundishaji na kuweza kupata matokeo mazuri.

Aidha Bw. Khamis amesema, ameridhishwa na kasi na utendaji wa walimu katika ufundishaji hali iliyopelekea kupata matokeo mazuri ya darasa la saba na darasa la Nne kwa mwaka wa masomo 2022/2023.

Pia , amewasisitiza walimu kusimamia nidhamu kwa walimu wao ili kuweza kuimarisha utendaji ulio bora maskulini.