{"id":2655,"date":"2026-08-21T07:45:15","date_gmt":"2026-08-21T07:45:15","guid":{"rendered":"https:\/\/moez.go.tz\/?p=2655"},"modified":"2026-08-21T08:04:19","modified_gmt":"2026-08-21T08:04:19","slug":"serikali-kuendelea-kuwekeza-katika-miundombinu-ya-elimu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/moez.go.tz\/?p=2655","title":{"rendered":"SERIKALI KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA MIUNDOMBINU YA ELIMU"},"content":{"rendered":"\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-1 wp-block-paragraph\">Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza dhamira yake ya kuendelea kutenga rasilimali za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora, salama na yanayochochea ujifunzaji.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-2 wp-block-paragraph\">Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Dakhalia la Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame, iliyofanyika katika viwanja vya skuli hiyo, Kibuteni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-3 wp-block-paragraph\">Balozi Dkt. Nchimbi amesema uwepo wa miundombinu imara ya kufundishia na kujifunzia ni msingi muhimu katika kuwaandaa vijana wenye ubunifu, maarifa na ujuzi utakaowawezesha kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-4 wp-block-paragraph\">Amesisitiza pia umuhimu wa Uongozi wa Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame kuhakikisha jengo hilo pamoja na miundombinu mingine ya skuli vinatunzwa na kulindwa kwa umakini ili viendelee kutoa huduma bora kwa wanafunzi na jamii kwa muda mrefu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-5 wp-block-paragraph\">Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha sekta ya elimu na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-6 wp-block-paragraph\">Amesema Wilaya ya Kusini Unguja imefanikiwa kwa asilimia 100 kuondoa mfumo wa mikondo miwili (double shift) katika skuli zake, hatua inayowawezesha wanafunzi kupata muda wa kutosha wa kujifunza na kushiriki kikamilifu katika shughuli za elimu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-7 wp-block-paragraph\">Habari njema kwa Wilaya hii ya Kusini Unguja ni kwamba tumeshafanikiwa kwa asilimia 100. Wanafunzi wote wa skuli kwenye Wilaya hii wanaingia mkondo mmoja,\u201d amesema Mhe. Lela.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-8 wp-block-paragraph\">Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mazingira ya elimu na kuongeza fursa za kujifunza kwa wanafunzi, huku ikizingatia pia muda wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya skuli na shughuli nyingine za malezi na elimu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-9 wp-block-paragraph\">LAPTOP 25 KUONGEZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-10 wp-block-paragraph\">Katika kuendelea kuimarisha elimu katika Mkoa wa Kusini Unguja, Mbunge wa Jimbo la Makunduchi na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ametoa laptop 25 kwa Uongozi wa Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-11 wp-block-paragraph\">Mhe. Wanu amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kuongeza fursa za kielimu kwa wanafunzi wa Mkoa wa Kusini Unguja, hususan katika matumizi ya teknolojia kama nyenzo muhimu ya kufundishia na kujifunzia.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-12 wp-block-paragraph\">Amesema matumizi ya teknolojia katika elimu yana nafasi kubwa katika kuwaandaa vijana kupata maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya dunia ya sasa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-13 wp-block-paragraph\">SHILINGI BILIONI 1.58 KUKAMILISHA UJENZI<br>Akitoa taarifa ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Jengo la Dakhalia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Asya Iddi Issa, amesema jumla ya Shilingi bilioni 1.58 zimetumika hadi kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-14 wp-block-paragraph\">Amesema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora na salama ya kujifunzia, huku ukilenga kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-15 wp-block-paragraph\">Aidha, amesema ujenzi wa miundombinu hiyo unatarajiwa kuchangia katika kuinua kiwango cha ufaulu, kuongeza mahudhurio ya wanafunzi, kuimarisha nidhamu pamoja na kuboresha ustawi wa wanafunzi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-16 wp-block-paragraph\">Bi. Asya amesisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya elimu ni uwekezaji wa muda mrefu unaoweka msingi imara wa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-17 wp-block-paragraph\">Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inaendelea kusimamia juhudi za Serikali katika kuhakikisha uwekezaji katika miundombinu, teknolojia na mazingira bora ya kujifunzia unaendana na azma ya kujenga mfumo wa elimu wenye ubora na unaowaandaa vijana kwa mahitaji ya dunia ya sasa.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-18 wp-block-paragraph\">Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano &#8211; WEMA<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza dhamira yake ya kuendelea kutenga rasilimali za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora, salama na yanayochochea ujifunzaji. Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Dakhalia la Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame, iliyofanyika katika viwanja vya skuli hiyo, Kibuteni, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja. Balozi Dkt. Nchimbi amesema uwepo wa miundombinu imara ya kufundishia na kujifunzia ni msingi muhimu katika kuwaandaa vijana wenye ubunifu, maarifa na ujuzi utakaowawezesha kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa. Amesisitiza pia umuhimu wa Uongozi wa Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame kuhakikisha jengo hilo pamoja na miundombinu mingine ya skuli vinatunzwa na kulindwa kwa umakini ili viendelee kutoa huduma bora kwa wanafunzi na jamii kwa muda mrefu. Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha sekta ya elimu na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Amesema Wilaya ya Kusini Unguja imefanikiwa kwa asilimia 100 kuondoa mfumo wa mikondo miwili (double shift) katika skuli zake, hatua inayowawezesha wanafunzi kupata muda wa kutosha wa kujifunza na kushiriki kikamilifu katika shughuli za elimu. Habari njema kwa Wilaya hii ya Kusini Unguja ni kwamba tumeshafanikiwa kwa asilimia 100. Wanafunzi wote wa skuli kwenye Wilaya hii wanaingia mkondo mmoja,\u201d amesema Mhe. Lela. Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mazingira ya elimu na kuongeza fursa za kujifunza kwa wanafunzi, huku ikizingatia pia muda wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya skuli na shughuli nyingine za malezi na elimu. LAPTOP 25 KUONGEZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA Katika kuendelea kuimarisha elimu katika Mkoa wa Kusini Unguja, Mbunge wa Jimbo la Makunduchi na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ametoa laptop 25 kwa Uongozi wa Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame. Mhe. Wanu amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kuongeza fursa za kielimu kwa wanafunzi wa Mkoa wa Kusini Unguja, hususan katika matumizi ya teknolojia kama nyenzo muhimu ya kufundishia na kujifunzia. Amesema matumizi ya teknolojia katika elimu yana nafasi kubwa katika kuwaandaa vijana kupata maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya dunia ya sasa. SHILINGI BILIONI 1.58 KUKAMILISHA UJENZIAkitoa taarifa ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Jengo la Dakhalia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Asya Iddi Issa, amesema jumla ya Shilingi bilioni 1.58 zimetumika hadi kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo. Amesema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora na salama ya kujifunzia, huku ukilenga kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, amesema ujenzi wa miundombinu hiyo unatarajiwa kuchangia katika kuinua kiwango cha ufaulu, kuongeza mahudhurio ya wanafunzi, kuimarisha nidhamu pamoja na kuboresha ustawi wa wanafunzi. Bi. Asya amesisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu ya elimu ni uwekezaji wa muda mrefu unaoweka msingi imara wa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inaendelea kusimamia juhudi za Serikali katika kuhakikisha uwekezaji katika miundombinu, teknolojia na mazingira bora ya kujifunzia unaendana na azma ya kujenga mfumo wa elimu wenye ubora na unaowaandaa vijana kwa mahitaji ya dunia ya sasa. Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano &#8211; WEMA<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":2657,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2655","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-latest_news"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2655","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=2655"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2655\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2659,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2655\/revisions\/2659"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2657"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=2655"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=2655"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=2655"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}