{"id":2197,"date":"2025-12-15T11:38:52","date_gmt":"2025-12-15T11:38:52","guid":{"rendered":"https:\/\/moez.go.tz\/?p=2197"},"modified":"2025-12-15T11:38:53","modified_gmt":"2025-12-15T11:38:53","slug":"mahafali-ya-kwanza-ya-kidato-cha-nne-skuli-ya-vivid-dream","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/moez.go.tz\/?p=2197","title":{"rendered":"MAHAFALI YA KWANZA YA KIDATO CHA NNE SKULI YA VIVID DREAM"},"content":{"rendered":"\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img fetchpriority=\"high\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"682\" src=\"https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92-1024x682.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-2198\" srcset=\"https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92-1024x682.jpg 1024w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92-300x200.jpg 300w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92-768x512.jpg 768w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92-18x12.jpg 18w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92-1200x800.jpg 1200w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.36_6903bb92.jpg 1280w\" sizes=\"(max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-4a9d46dacc1ae096e0bbb6cab8448351 wp-block-paragraph\">Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdullah Said, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Skuli binafsi ambazo zinatoa fursa Mbadala kwa watoto wa jamii ya kizanzibari na kutambua umuhimu wa skuli hizo kwa kuwaandaa vijana kuendana na mabadiliko ya dunia yanayoendelea kubadilika kwa kasi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-b618afc2b2c393e164c8433e26b5e008 wp-block-paragraph\">Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wizara ya elimu Zanzibar Naibu katibu Mkuu Utawala Ndugu Amos John Henock wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Skuli ya Vivid Dream yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Nkrumah, Mfenesini Wilaya ya Magharibi A Unguja.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-4df30c9b63e087edef5a4845cac9dc12 wp-block-paragraph\">Ndugu Amos amewakumbusha wazazi na walezi kuwa jambo la msingi linalosaidia kwa kiasi kikubwa katika kutoa Elimu kwa watoto wetu ni kulipa ada kwa wakati kwani uendeshaji wa skuli hizo unahitaji rasilimali mbalimbali ili kutoa huduma bora na kufikia malengo wanayojipangia.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-285cc6cda181e8246088c3ab8f784279 wp-block-paragraph\">Aidha, naibu katibu mkuu amebainisha kuwa Wizara ya Elimu kwa sasa imepanua wigo na ufadhili wa Elimu ya Juu hadi kuwafikia wanafunzi wa Diploma hivyo ni jukumu la wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuzipata fursa hizo.<\/p>\n\n\n\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"682\" src=\"https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b-1024x682.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-2199\" srcset=\"https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b-1024x682.jpg 1024w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b-300x200.jpg 300w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b-768x512.jpg 768w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b-18x12.jpg 18w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b-1200x800.jpg 1200w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-15-at-13.39.37_2b5c139b.jpg 1280w\" sizes=\"(max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-c0344586f979849eebaa7bda97f6a5a1 wp-block-paragraph\">Mapema bwana Henok amesema Taasisi ya Nur Alyaqeen Foundation inaunga mkono jihudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hususan katika masuala ya Huduma za Kijamii ikiwemo huduma za kielimu na afya.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-6293e6739a5fdf80b2532db95fcc99dd wp-block-paragraph\">Aidha ameushauri uongozi wa skuli binafsi kuweka ajira za kudumu zenye mikataba inayofahamika ambazo zitakuwa na mustakbali mwema kwa wafanyakazi ili kuwa na imani na amani muda wote wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi zao za kila siku.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-912c70720cc2d7c248ebbc309cfd3c6d wp-block-paragraph\">Akimkaribisha mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndugu Subira Abdalla Vuai ameipongeza skuli ya VIVID kwa Kuandaa vyema kahafali yao ya kwanza kwa kidato cha nne na kuishukuru jumuiya ya skuli binafsi kwa kuendelea kutoa taaluma na kuipunguzia mrundikano wa wanafunzi katika skuli za Serikali.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-d7ed679eff0fc86a22e11889bece8f03 wp-block-paragraph\">Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Nur Alyaqeen Foundation (NAYF) ambayo ndiyo mlezi wa Skuli ya Vivid Ndugu Makame Salim Ali akitoa historia ya Tasisi hiyo amesema kuwa Taasisi ya NAYF ilianzishwa mwaka 2016 na kusajiliwa rasmi mwaka 2017 baada ya wana jamii kuungana na kuona iko haja ya kuwa na Taasisi madhubuti itakayosimamia masuala mbalimbali kwenye jamii yetu yakiwemo masuala ya Kielimu chini ya kauli mbiu isemayo &#8220;NAYF for faith education and humanitarian services&#8221;. Ikiwa na malengo ya kuwaandaa vijana kuwa wazalendo wa nchi yao.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-d9bdfdee1afcd2dd9ffd9a8d0966e569 wp-block-paragraph\">Alibainisha kuwa dunia ya leo inahitaji watu majasiri na wenye maono hivyo amewataka wahitimu na wanafunzi kwa ujumla kushikamana na mafunzo waliopatiwa wakiwa shuleni hapo ili kuibadilisha jamii kufikia ustawi ulio bora.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-b21e5ae6ab0556c050a346995523434f wp-block-paragraph\">Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na&nbsp;Uhusiano,&nbsp;WEMA.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdullah Said, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Skuli binafsi ambazo zinatoa fursa Mbadala kwa watoto wa jamii ya kizanzibari na kutambua umuhimu wa skuli hizo kwa kuwaandaa vijana kuendana na mabadiliko ya dunia yanayoendelea kubadilika kwa kasi. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wizara ya elimu Zanzibar Naibu katibu Mkuu Utawala Ndugu Amos John Henock wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Skuli ya Vivid Dream yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Nkrumah, Mfenesini Wilaya ya Magharibi A Unguja. Ndugu Amos amewakumbusha wazazi na walezi kuwa jambo la msingi linalosaidia kwa kiasi kikubwa katika kutoa Elimu kwa watoto wetu ni kulipa ada kwa wakati kwani uendeshaji wa skuli hizo unahitaji rasilimali mbalimbali ili kutoa huduma bora na kufikia malengo wanayojipangia. Aidha, naibu katibu mkuu amebainisha kuwa Wizara ya Elimu kwa sasa imepanua wigo na ufadhili wa Elimu ya Juu hadi kuwafikia wanafunzi wa Diploma hivyo ni jukumu la wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuzipata fursa hizo. Mapema bwana Henok amesema Taasisi ya Nur Alyaqeen Foundation inaunga mkono jihudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hususan katika masuala ya Huduma za Kijamii ikiwemo huduma za kielimu na afya. Aidha ameushauri uongozi wa skuli binafsi kuweka ajira za kudumu zenye mikataba inayofahamika ambazo zitakuwa na mustakbali mwema kwa wafanyakazi ili kuwa na imani na amani muda wote wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi zao za kila siku. Akimkaribisha mgeni rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndugu Subira Abdalla Vuai ameipongeza skuli ya VIVID kwa Kuandaa vyema kahafali yao ya kwanza kwa kidato cha nne na kuishukuru jumuiya ya skuli binafsi kwa kuendelea kutoa taaluma na kuipunguzia mrundikano wa wanafunzi katika skuli za Serikali. Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Nur Alyaqeen Foundation (NAYF) ambayo ndiyo mlezi wa Skuli ya Vivid Ndugu Makame Salim Ali akitoa historia ya Tasisi hiyo amesema kuwa Taasisi ya NAYF ilianzishwa mwaka 2016 na kusajiliwa rasmi mwaka 2017 baada ya wana jamii kuungana na kuona iko haja ya kuwa na Taasisi madhubuti itakayosimamia masuala mbalimbali kwenye jamii yetu yakiwemo masuala ya Kielimu chini ya kauli mbiu isemayo &#8220;NAYF for faith education and humanitarian services&#8221;. Ikiwa na malengo ya kuwaandaa vijana kuwa wazalendo wa nchi yao. Alibainisha kuwa dunia ya leo inahitaji watu majasiri na wenye maono hivyo amewataka wahitimu na wanafunzi kwa ujumla kushikamana na mafunzo waliopatiwa wakiwa shuleni hapo ili kuibadilisha jamii kufikia ustawi ulio bora. Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na&nbsp;Uhusiano,&nbsp;WEMA.<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":2200,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2197","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-latest_news"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2197","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=2197"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2197\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2201,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2197\/revisions\/2201"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2200"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=2197"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=2197"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=2197"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}