{"id":2035,"date":"2025-12-04T06:36:56","date_gmt":"2025-12-04T06:36:56","guid":{"rendered":"https:\/\/moez.go.tz\/?p=2035"},"modified":"2025-12-04T08:39:05","modified_gmt":"2025-12-04T08:39:05","slug":"mhe-hemed-atoa-miongozo-itakayoimarisha-utendaji-kazi-katika-sekta-ya-elimu-zanzibar","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/moez.go.tz\/?p=2035","title":{"rendered":"MHE: HEMED ATOA MIONGOZO ITAKAYOIMARISHA UTENDAJI KAZI KATIKA SEKTA YA ELIMU ZANZIBAR."},"content":{"rendered":"\n<figure class=\"wp-block-image size-large\"><img fetchpriority=\"high\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"683\" src=\"https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-04-at-09.48.10_47acfbef-1024x683.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-2043\" srcset=\"https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-04-at-09.48.10_47acfbef-1024x683.jpg 1024w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-04-at-09.48.10_47acfbef-300x200.jpg 300w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-04-at-09.48.10_47acfbef-768x512.jpg 768w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-04-at-09.48.10_47acfbef-18x12.jpg 18w, https:\/\/moez.go.tz\/wp-content\/uploads\/2025\/12\/WhatsApp-Image-2025-12-04-at-09.48.10_47acfbef.jpg 1080w\" sizes=\"(max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><\/figure>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-df5864734e865946f56eed1e8638ccd6 wp-block-paragraph\">Viongozi na watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuangalia vipaombele vya Wizara ya Elimu vilivyoainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2030, Dira ya Maendeleo ya 2050 na Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-2d60811b66cd8b5fd8115145d838a820 wp-block-paragraph\">Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati alipokutana na kutoa miongozo kwa viongozi wa ngazi mbali mbali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-157ac46b255ab9596af9a33a5aa7e52a wp-block-paragraph\">Amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2030 imeainisha mambo mahsusi ya kutekelezwa na Wizara ya Elimu pamoja na Hotuba ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi aliyoitoa katika uzinduzi wa Baraza la 11 la Wawakilishi imefafanua vipaombele vya Serikali vya kutekelezwa na Sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Elimu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-58a8cde3528b517ccb96632274e54946 wp-block-paragraph\">Mhe. Hemed amesema ili kufanikiwa kutekeleza mipango na mikakati ya Wizara iliyojipangia ni lazima viongozi wakasimamia suala la nidhamu na uwajibikaji kwa walimu na watumishi wengine ili kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-48822bcba2d7ef665400c5aaa8130c19 wp-block-paragraph\">Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza kuwepo kwa matumizi mazuri ya fedha na usimamizi wa mali za Serikali, sambamba na kuheshimu taratibu za ujazwaji wa mikataba ili kuweza kupata miradi yenye viwango bora.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-464a3ed5f9a1cbb559e502438d951cc2 wp-block-paragraph\">Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka Wakurugenzi wa Wizara hiyo kufanya ufuatiliaji katika maeneo yao wanayoyaongoza ili kubaini changamoto mbali mbali zinazojitokeza na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-e4a692b8b866e49eb486239120ca6c74 wp-block-paragraph\">Mhe. Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kusimamia haki, maslahi na stahiki za watumishi na kuharakisha uundwaji wa Tume ya Utumishi ya Walimu itakayosimamia maslahi na nidhamu za walimu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-6c08895c863a12083e0d5d7efa1d5936 wp-block-paragraph\">Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Nane kwa kuendelea kuipa kipaombele sekta ya elimu kuanzia ngazi ya Maandalizi hadi Vyuo Vikuu.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-1123a088fe6c83e581de55835ba420b2 wp-block-paragraph\">Aidha, Waziri Lela amesema viongozi na watendaji wa Wizara ya elimu wapo tayari kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yote yanayotolewa na Serikali yenye lengo la kukuza na kuimarisha sekta ya Elimu nchini.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"has-text-align-left has-black-color has-text-color has-link-color wp-elements-4c61eb33e210ff1e816c8ec4841e75a6 wp-block-paragraph\">Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Tarehe:&nbsp;03\/12\/2025.<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\"><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Viongozi na watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuangalia vipaombele vya Wizara ya Elimu vilivyoainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2030, Dira ya Maendeleo ya 2050 na Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar. Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati alipokutana na kutoa miongozo kwa viongozi wa ngazi mbali mbali kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwenye kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi. Amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2030 imeainisha mambo mahsusi ya kutekelezwa na Wizara ya Elimu pamoja na Hotuba ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi aliyoitoa katika uzinduzi wa Baraza la 11 la Wawakilishi imefafanua vipaombele vya Serikali vya kutekelezwa na Sekta mbali mbali ikiwemo Sekta ya Elimu. Mhe. Hemed amesema ili kufanikiwa kutekeleza mipango na mikakati ya Wizara iliyojipangia ni lazima viongozi wakasimamia suala la nidhamu na uwajibikaji kwa walimu na watumishi wengine ili kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza kuwepo kwa matumizi mazuri ya fedha na usimamizi wa mali za Serikali, sambamba na kuheshimu taratibu za ujazwaji wa mikataba ili kuweza kupata miradi yenye viwango bora. Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka Wakurugenzi wa Wizara hiyo kufanya ufuatiliaji katika maeneo yao wanayoyaongoza ili kubaini changamoto mbali mbali zinazojitokeza na kuzipatia ufumbuzi wa haraka. Mhe. Hemed ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kusimamia haki, maslahi na stahiki za watumishi na kuharakisha uundwaji wa Tume ya Utumishi ya Walimu itakayosimamia maslahi na nidhamu za walimu. Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed Mussa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Nane kwa kuendelea kuipa kipaombele sekta ya elimu kuanzia ngazi ya Maandalizi hadi Vyuo Vikuu. Aidha, Waziri Lela amesema viongozi na watendaji wa Wizara ya elimu wapo tayari kuyafanyia kazi maagizo na maelekezo yote yanayotolewa na Serikali yenye lengo la kukuza na kuimarisha sekta ya Elimu nchini. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Tarehe:&nbsp;03\/12\/2025.<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":2041,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-2035","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-latest_news"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2035","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=2035"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2035\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":2044,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/2035\/revisions\/2044"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/2041"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=2035"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=2035"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/moez.go.tz\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=2035"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}