
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema kuwaandaa Wanafunzi kimasomo kutapelekea kuzalisha wataalamu wenye ufanisi katika fani mbalimbali nchini.
Amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya hatua ya kwanza ya kuwaandaa Wanafunzi wa afya huko Zanzibar school of health ZSH Kwa Mchina Mwanzo Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Amesema kumuandaa Mwanafunzi mapema kimasomo ni kumjengea mustakabali mwema katika maisha yake ya Chuo Kwa kipindi chote Cha masomo.
Aidha Mhe Gulam amesema, Wizara ya Elimu kupitia Bodi ya Mikopo iko mbioni kurekebisha Sheria za mkopo ili na wanafunzi wa diploma na waweze kunufaika na mikopo hiyo. Amesema hatua hiyo itasaidia vijana wengi nao kuweza kutumia fursa za masomo.