
KUFUNGA KIKAO CHA TATHMINI YA NUSU MWAKA YA MRADI WA KUIMARISHA UBORA WA ELIMU YA SEKONDARI ZANZIBAR
- Details
- 67
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Khamis Abdulla Said amesema, ni muda sasa kwa kila mwalimu kuchukua hatua ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kupata matokeo mazuri zaidi.
Amesema hayo wakati wa kufunga kikao cha tathmini ya nusu mwaka ya Mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar, Katika ukumbi wa mikutano Golden Tulip uwanja wa ndege Mjini Unguja.
Amesema, ili Walimu waendelee kufanya kazi kwa juhudi kubwa Wizara itaendelea kufanya kila namna kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Walimu nao wanaendelea kupewa Mafunzo ili kuendana na mabadiliko ya Teknolojia.
Amesema, Zanzibar ili iendelee kupata matokeo mazuri ipo haja ya kila muhisika kutimiza wajibu wake kwa kuengeza bidii zaidi.