Title Image

Semina ya Walimu

news phpto

Naibu wa Waziri wa Elimu Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akiwahutubia walimu jkatika semina elekezi juu ya usimamizi wa mitihani ya Taifa hapo katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasie

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri amewasisitiza Walimu kujali muda wa kazi, Umakini, Kutunza siri na uaminifu katika mitihani itakayoanza hivi karibuni katika skuli za Unguja na Pemba.

Mhe. Mjawiri ameyasema hayo leo katika ukumbi wa skuli ya Sekondari ya Haile salassie alipokuwa akifungua semina elekezi kwa wasimamizi wa mitihani ya Taifa ya darasa la nne, Sita na kidato cha pili itakayoanza tarehe 20/11 hadi 6/11/2017.

Pia Mhe, Mjawiri amewataka walimu hao kujiepusha na vitendo vya udanganyifu katika usimamizi wa mitihani hiyo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Nae Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani Nd, Zubeir Juma Khamis amewasisitiza walimu hao kufuata Sheria na kanuni katika kazi ya usimamizi wa mitihani hiyo na kwamba yoyote atakayekwenda kinyume na kanuni za mitihani, Baraza halitosita kumchukulia hatua zinazostahiki.