Title Image

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR MHE. MMANGA MJENGO MJAWIRI ATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WARSHA YA KUANDAA MPANGO WA MAENDELEO YA ELIMU WA ZANZIBAR, KAMA IFUATAVYO:

Ndugu Wananchi,

Ndugu Wazazi,

Ndugu Walimu na wanafunzi,

Wizara inachukua fursa hii kuwaarifu wananchi kuwa imeandaa warsha ya siku tano kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Elimu wa Zanzibar itakayofanyika kuanzia Jumatatu tarehe 8 Agosti 2016 hadi Ijumaa tarehe 12 Agosti 2012 katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mkoa Mjini wa Magharibi, Unguja. Warsha hiyo itahudhuriwa na washiriki 90 kutoka katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vilivyopo Zanzibar, Washirika wa Maendeleo wakiwemo ‘Global Partnership for Education’ (GPE), Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Shirika la Misaada la Kimataifa la Sweden (Sida), Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID), UNICEF na UNESCO. Aidha mashirika mbali mbali yasio ya kiserikali yanayoshughulikiwa na elimu yakiwemo Milele Zanzibar Foundation, Aga Khan, Madrassa Early Childhood Programme, FAWE, ZAPDD, Bodi za Elimu na Kamati za Skuli, Wakuu wa Vituo vya Walimu, Walimu Wakuu na Wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali za Unguja na Pemba pia watashiriki warsha hiyo.

PATA TAARIFA KAMILI