Title Image

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR YAPONGEZA MAENDELEO YA MRADI WA TUSOME PAMOJA

news phpto

Afisa Mdhamini Elimu na Mafunzo ya Amali Ndugu Salim Kitwana Sururu wakati alipozungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika kikao cha kutathmini utekelezaji wa mradi Tusome Pamoja kwa mwaka 2017 na matayarisho ya mapango kazi kwa mwaka 2018

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar yaonesha kuridhishwa na maendeleo ya mradi wa Tusome Pamoja uliopo chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Marekani USAID. Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini Elimu na Mafunzo ya Amali Ndugu Salim Kitwana Sururu wakati alipozungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar katika kikao cha kutathmini utekelezaji wa mradi huo kwa mwaka 2017 na matayarisho ya mapango kazi kwa mwaka 2018 katika kikao kilichofanyika huko Morogoro Tanzania tarehe 5-6 Disemba, 2017.

Ndugu Salim amelishukuru shirika la USAID kwa mchango mkubwa walioutoa kwa Zanzibar na Tanzania katika sekta ya elimu. Mradi huu umejikita katika ngazi ya msingi chini darasa la kwanza hadi la nne. Miongoni mwa shughuli zinazofanya na mardi huu ni: (Kusaidia wanafunzi kuweza kusoma kuandinka na kuhesabu (KKK); kutoa mafunzo kwa walimu wa ngazi ya Msingi Chini juu ya mbinu bora za ufundishaji na matumizi bora ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ubunifu katika kutengeneza vifaa vya kujifundishia kutoka katika mazingira yaliyo wazunguka tena kwa gharama nafuu, kuanzisha ushirikiano kati ya jamii na walimu “UWAWA” ambao wanasaidia watoto na kuweka kikao cha kila mwezi kujadili mafanikio na changamoto zilizopo na hatimae kuziwasilisha kwa kamati ya skuli kwa hatua. Pia, mradi umesaidia vitabu ambavyo kila mwanafunzi anapatiwa nakala yake, pia wataalamu wetu kujengewa uwezo wa kutunga vitabu vinavyosadia kufujinza na kufundishia kwa mashirikiano na Taasisi za Elimu Zanzibar na Tanzania (ZIE na TIE).

Kwa ujumla maendeleo yanaridhisha sana. Kama kila mtu atawajibika kwa nafasi yake bila shaka ufaulu utaongezeka katika skuli na hatimae kwa Taifa kwa ujumla. Mradi huu unatelezwa katika mikoa minne kwa upande wa Tanzania Bara (Iringa, Morogoro, Mtwara na Ruvuma) na mikoa yote ya Zanzibar.