Title Image

MAPOKEZI YA MHE, WAZIRI NA MHE, NAIBU WAZIRI WA ELIMU WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI, SIKU YA TAREHE 12/04/2016

news phpto

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma akiwsili kwa mara ya kwanzza katika Makao Makuu ya Wizara tangu kushika Wadhifa huo

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Riziki Pembe Juma akifuatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri wameripoti rasmi katika Ofisi zao leo hii tarehe 12 April, 2016 tayari kwa kuanza kazi.

Waliowasili katika eneo hilo la Makao Makuu Wizara Mazizini walipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Bibi. Khadija Bakari Juma na Naibu Katibu Mkuu Taaluma Bibi, Madina Mjaka Mwinyi , wakurugenzi mbali mbali wa Idara na Taasisi za Wizara ya Elimu zinazojitegemea, Maafisa na watendaji waliopo Makao makuu ya Wizara, kwa pamoja tunawakaribisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na kuwatakia kila la kheri katika uongozi wao.

Baada ya mapokezi hayo walifika kwenye ofisi zao na baadae kuingia kwenye ukumbi wa mkutano wa Wizara, ukiwa ni mkutano wao wa kwanza na watendaji wa Wizara ambao pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu, Naibu Katibu –Taaluma, Wakurugenzi wa Idara, Taasisi, Mamlaka, Mashirika, Bodi na Vitengo tofauti vya Wizara ya Elimu. Katibu Mkuu aliwakaribisha viongozi hawa na kutoa muhtasari wa shughuli za Wizara , muundo na baadae kutoa fursa kwa washiriki kujitambulisha kila mmoja na kuelezea miundo wa Taasisi zao pamoja na majukumu yao.

Mhe, Naibu Waziri wa Elimu Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri aliwasalimu washiriki wa mkutano huo na kuelezea kwamba :-

1. Katika utekelezaji wa kazi zao itakuwa ni vyema kuwajua wasaidizi wao katika utendaji, kujua kazi zao pamoja na kujua mazingira wanayoyafanyia kazi kwa upana zaidi.

2. Alisisitiza kufanya kazi kwa pamoja huku tukiongozwa na kauli mbiu “ELIMU BORA KWANZA”

3. Kuhakikisha kwamba mitaala iliyokuwepo inakidhi haja ili kufikia lengo la kauli mbiu husika.

4. Kushirikia na walimu, wanafunzi na wazazi katika kuendeleza ubora wa elimu nchini .

5. Kusimamia upatikanaji wa vifaa na nyenzo za kujifunzia na kufundishia.

6. Kuingiza katika mpango wa utekelezaji wa Elimu vipaumbele vyote vya Elimu vilivyotajwa na Mhe, Rais katika hotuba ya kulifungua Baraza la Wawakilishi.

7. Kuwasimamia walimu ili wafanyekazi zao kwa kufuata maadili na miiko ya kazi ya ualimu.

Alimalizia kwa kusema kwamba kazi iliyo mbele yetu ni kuleta mashirikiano ya dhati katika kutekeleza majukumu tuliyopewa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe, Riziki Pembe Juma alitoa shukrani za dhati kwa Mhe, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein kwa uteuzi aliofanya kuwateua wao Mhe, Waziri na Mhe, Naibu Waziri kuongoza Wizara hii ambapo kwa pamoja wanaifahamu Wizara kwa kiasi fulani lakini yapo mengi ya kujifunza hasa katika masuala ya uendeshaji na utawala ukizingatia ukubwa wa Wizara yetu.

Aidha, alisisitiza yafuatayo:-

1. Kuwajua wasaidizi wao katika utendaji, kujua kazi zao pamoja na kujua mazingira wanayoyafanyia kazi.

2. Kufanya kazi kwa pamoja huku tukiongozwa na kauli mbiu ya “ELIMU BORA KWANZA” ili kufikia matarajio ya wananchi ambao ndio mwelekeo wa Mheshimiwa, Rais wa Zanzibar.

3. Kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo ya Elimu nchini.

4. Amesisitiza kuwa watendaji zaidi kuliko wasemaji.

Hitimisho.

Kabla Mwenyekiti kuahirisha kikao Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali aliwapongeza Mhe, Waziri na Naibu Waziri kwa kusema kwa mara nyengine tena kwa niaba ya Wizara “tunawapongeza Mheshimiwa Waziri kwa uteuzi wa kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe, Riziki Pembe Juma na Naibu Waziri Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri na kuwaahidi kuwapa mashirikiano ili kauli mbiu ya ‘ ELIMU BORA KWANZA’ liweze kufikiwa.