Title Image

TANGAZO LA NAFASI MBALIMBALI ZA MASOMO.

Posted: 2018-01-04 22:21:21
Chuo Kikuu cha Maastricht kilichopo Uholanzi kinatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kutoka mataifa yanayoendelea wanaotaka kujiunga na chuo hicho.
Ufadhili huu ni kwa wale wanaotaka kujiendeleza na Shahada ya Uzamili katika kozi mbalimbali zinatolewa chuoni hapo.
Masharti
 Mwombaji hatakiwi kuwa na uraia wa nchi yoyote iliyo chini ya jumuiya ya Ulaya
 Mwombaji anatakiwa awe ametimiza vigezo vya kujiunga na chuo kikuu cha Maastricht kabla ya kuomba ufadhili.
 Mwombaji hatakiwi kuwa amepitia ngazi yoyote ya elimu nchini Uholanzi.
 Umri usizidi miaka 35.
 Waombaji wenye ufaulu mkubwa watapewa kipaumbele.

Kwa maelezo zaidi tafdhali tembelea anuani hii: TANGAZO LA NAFASI MBALIMBALI ZA MASOMO. 2017/2018